FISTON MAYELE amemaliza mkataba wake na timu ya Pyramids na kwa taarifa za awali mchezaji huyo hatokuwepo kwenye kampeni za Pyramids msimu ujao.
Klabu ya Al Fateh inayoshiriki ligi kuu ya Saudi Arabia, imeweka nia ya kumsajili Mayele, na mipango hiyo imeshaanza, Muda wowote kuanzia sasa Fiston Mayele atasaini kandarasi na timu hiyo ya Saudi Arabia.
Inaelezwa kuwa uongozi wa Pyramids haujaridhishwa na maamuzi ya Mayele kwa kuwa bado wanahitaji huduma yake kama mshambuliaji.