Katika mbio za ufungaji bora, kiungo wa Simba, Jean Charles Ahoua ameendelea kuwakimbia washambuliaji wa Yanga, Clement Mzize na Prince Dube.
Ahoua amefikisha mabao 16 baada ya kufunga moja dhidi ya KenGold, akiwaacha matatu Mzize na Dube wenye 13 huku wachezaji wote hao wakibakiwa na michezo miwili kuhitimisha msimu huu ambapo Juni 25 timu zao zitakutana zenyewe.
Kina Mzize wanahitaji kufunga mabao matatu kila mmoja ili kumng’oa Ahoua kileleni ikiwa hatafunga katika mechi mbili zijazo kwani staa huyo wa Simba ana penalti nyingi ukilinganisha na nyota hao wawili wa Yanga