Dabi ya Kariakoo ni moja ya michezo mikubwa na yenye mvuto zaidi katika soka la Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki, ambapo hushuhudia upinzani mkali kati ya klabu kongwe zenye mashabiki wengi nchini. Kwa kuzingatia ukubwa wa mchezo huu, hatua ya TPLB kuleta waamuzi wa kimataifa inalenga kuongeza imani kwa wadau wote wa soka, wakiwemo wachezaji, makocha, viongozi na mashabiki.
Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa kuanzia saa 11:00 jioni na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na nafasi za juu za msimamo wa ligi na historia ndefu ya upinzani kati ya klabu hizi mbili.
Mashabiki wa soka nchini na nje ya mipaka wanahimizwa kufika uwanjani kwa wingi kwa kufuata taratibu zote za kiusalama, huku vyombo husika vikiwa tayari kuhakikisha hali ya utulivu na nidhamu inatawala ndani na nje ya uwanja siku ya mchezo.
Bodi ya Ligi Kuu ya soka nchini Tanzania bara TPLB hatimaye imetoa orodha ya waamuzi wa dabi ya Kariakoo. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, TPLB imetangaza maofisa wa mchezo wa dabi ya Kariakoo kwenye Ligi Kuu bara ya wenyeji Young Africans SC na Simba SC. Mechi hiyo ya nambari 184 itachezwa na waamuzi kutoka Misri. Jambo ambalo limezua mijadala mbalimbali mitandaoni.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, mwamuzi wa kati atakuwa Amin Mohammed Amin Omar kutoka Misri. Mwamuzi huyu atasaidiwa na Mohammed Ahmed Abo El Regal kama mwamuzi msaidizi namba moja na Samir Gamal Saad Mohammed ambaye atakuwa msaidizi namba 2.