Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam imeshindwa kwenye kesi yake ya awali iliyoifungua kwenye Mahakama ya Usuluhishi Michezoni (CAS).
Yanga SC katika kesi ya msingi ikiyoifungua dhidi ya TFF, Bodi ya Ligi na Simba SC imeomba kupewa alama 3 na mabao 3, lakini ikaiomba CAS pia izuie tarehe ya ‘DABİ’ isipangwe mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa, yani ile ya kudai alama 3 na mabao 3 kwa walichosema Simba SC waligomea mchezo wa tarehe 8 Machi,2025.
Walalamikiwa Simba SC, TFF na Bodi ya Ligi kwenye utetezi wao walipinga Yanga SC kufungua kesi CAS na kuzivuka mamlaka za TFF za kisheria.
Kwenye hukumu CAS wamekubaliana na Simba SC, TFF na Bodi ya Ligi kwamba wao CAS hawana mamlaka ya kuzuia kupangwa kwa tarehe ya DABI, lakini pia wamekubaliana na walalamikiwa kwamba wao CAS hawana pia ya kushughulikia jambo hili kabla halijapitia kwenye mamlaka za kisheria za TFF.
Hivyo basi shauri la Yanga SC limepigwa chini na sasa TFF na BODI YA LİGİ wako huru kupanga tarehe ya DABI na itapigwa kama kawaida.
Kwa hukumu hii Yang SC wakigomea kucheza DABI itakapopangwa, maana yake ni kwamba watapokonywa alama 15, wako tayari kwa hilo? Msimamo wao ulikuwa hakuna kucheza hiyo mechi lakini walikuwa wanategemea CAS ambako wamepigwa za uso tena pamoja na lundo na mawakili walio orodheshwa huko CAS. Dabi haina kipengele, kipengele uje nacho wewe.