Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Klabu 6 za EPL zamtaka Jonathan David

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Klabu 6 za EPL zamtaka Jonathan David


Atletico Madrid wameweka beki wa Tottenham raia wa Argentina, Cristian Romero, 27, kama moja ya wachezaji itakaowasajili msimu huu wa joto. (Marca)


Manchester City wanatarajiwa kumsajili beki wa pembeni wa Juventus na Italia, Andrea Cambiaso, 25, huku klabu hiyo ya Italia ikielekeza macho yake kwa beki wa Arsenal raia wa Ureno, Nuno Tavares, 25, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Lazio. (Sun)


Newcastle United, Manchester United, Tottenham, West Ham, Chelsea na Liverpool zote zinamwania mshambuliaji wa Canada Jonathan David, 25, ambaye mkataba wake na Lille unamalizika msimu wa joto, lakini Marseille wanajaribu kumshawishi aendelee kubaki Ufaransa. (RMC sports)


Manchester United wamempa mshambuliaji wa Wolves, Matheus Cunha, mkataba wa miaka mitano iwapo Mbrazi huyo mwenye umri wa miaka 25 ataamua kuhamia Old Trafford. (Teamtalk)


Chelsea wanajitahidi kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Juventus, Kenan Yildiz, 19, lakini wanakutana na ushindani kutoka Arsenal, Liverpool, Manchester United na Manchester City wanaomtaka pia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki. (Caught Offside)


Manchester United bado wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace raia wa Ufaransa, Jean-Philippe Mateta, 27, iwapo watashindwa kumchukua mshambuliaji wa Ipswich Town raia wa Uingereza, Liam Delap, 22. (GiveMeSport)


Newcastle United wanafanyia kazi dili la kumsajili beki wa kimataifa wa Korea Kusini, Kim Min-jae, 28, kutoka Bayern Munich msimu huu wa joto. (Football Insider)


Orodha ya Newcastle ya wachezaji inaowataka kuimarisha safu yao ya ulinzi pia inajumuisha Ousmane Diomande wa Sporting, mwenye umri wa miaka 21 kutoka Ivory Coast, Malick Thiaw wa AC Milan, beki wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23, na Jan Paul van Hecke, 24, kutoka Brighton. (GiveMeSport)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad