Azam Fc imesukumizwa nje ya michuano ya kombe la Muungano 2025 kufuatia kipigo cha 2-1 dhidi ya JKU FC ya Zanzibar kwenye nusu fainali. Mfungaji wa bao la pili la JKU Fc, Fred Sliman amechaguliwa kuwa nyota wa mchezo na anachukua zawadi yake kutoka City Institute of Health, Dar es Salaam.
JKU Fc imetinga fainali kumsuburi mshindi kati ya Zimamoto Fc dhidi ya Wananchi, Young Africans Sc watakaochuana kesho.
FT: JKU FC 2-1 AZAM FC
⚽ 50’ Neva Adelin
⚽ 80’ Fred Sliman
⚽ 15’ Yeison Fuentes
Azam Fc msimu huu wametolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, kombe la Shirikisho la CRDB na hata Ligi Kuu hawana uwezo wa kuchukua kwa kuwa hata wakishinda mechi zote zilizosalia hawawezi kuzifikia pointi za vinara wa Ligi Yanga Sc.