Nimewafatilia sana Stellenbosch ambao watakutana na Simba hatua ya Nusu Fainali CAFCC ….. hawa wababe kutoka South Africa 🇿🇦 wapo kwenye msimu bora sana (Nafasi ya tatu kwenye ligi nyuma ya Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates) .
Stellenbosch wana Fullback wao anaitwa Fawaaz Basadien moja ya mchezaji mzuri sana , uwezo mkubwa wa kushambulia na kutengeneza nafasi eneo la mbele then defense yupo vizuri pia .
DEVIN TITUS “Player to watch” anacheza kama winger wa kushoto 🔥 Nafikiri huyu mwamba ni wakumuangalia sana … anaweza kuathiri mchezo kwa kiasi kikubwa sana ( 1 vs 1 ngumu kukabiliana nae) .
Stellenbosch msimu huu kwenye mashindano ya CAF wamepoteza michezo mitatu kwenye hatua ya Group stage yote dhidi ya Rs Berkane (Home and Away) na dhidi ya Stade Malien .
Sio mchezo rahisi kwa Lunyasi kutokana na form ya Stellenbosch kwasasa ✍️