Mlinzi wa Simba Che Malone Fondoh ameweka wazi kuwa eneo la kuchezea [pitch] la uwanja wa New Amaan huenda likawa changamoto lakini hakuna namna wachezaji watacheza kwa sababu kuna viwanja ambacho si rafiki kwenye mechi za Ligi Kuu wamekuwa wakicheza na kumudu.
Amesisitiza kuwa wanatakiwa kufunga magoli mengi kadiri inavyowezekana huku wakihakikisha hawafungwi goli, hata ikitokea wameruhusu gaoli basi wao wanapaswa kufunga magoli zaidi.
Umakini wakati wote wa mchezo ndio kitu kinachotakiwa huku wakicheza mchezo ambao wao wamezoea kucheza.