Mobile

Haji Manara Afunguka Kwa Uchungu Baada ya Simba Kutinga Fainali CAF

Haji Manara Afunguka Kwa Uchungu Baada ya Simba Kutinga Fainali CAF



Aliyekuwa msemaji wa Simba ambaye kwa Sasa amehamia yanga SC Haji manara ameipongeza timu ya Simba Sc kwa kufika hatua ya Fainali na kuwataka Mashabiki wa Yanga Sc Waache Kununa ila wajipange kwa Kufanya vizuri Kombe la Klabu Bingwa Mwakani

Manara Amendika ujumbe wake kwakusema Kwa nature ya Ushabiki wetu hapa nchini ni ngumu sana kwetu kupokea uchungu huu Lakini hiyo ndio football,jana kwetu leo ni kwao!, Na wala sio mwisho wa dunia kwa wao kufika finali ya kombe la looser Tujipange kwa Champions league ya msimu ujao na tukavuke malengo yetu Haya ya kujinunisha ni kujitia Stress bila sababu Waacheni watambe na ndio raha ya Utani wetu wa jadi. - Manara

Simba SC ya Tanzania imetinga fainali katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya stelnoboch ya Afrika kusini baada ya kutoa sare katika mchezo wa vuta ni kuvute na kuwa na faida ya goli la mchezo wa kwanza lililofungwa na jean chales ahoua.



Katika mchezo huo Kipindi Cha kwanza kilimalizika kwa timu zote Bila kufungana ambapo pia kulikuwa na matukio ya kushangaza likiwemo lile la kibu Denis kuchezewa ndivyo sivyo lakini VAR ilikataa kwamba sio penati na kufanya mchezo kuendelea kuchezwa na hatimaye kwenda dakika 45 Bila ya yeyote kuibuka mbabe.

Kipindi Cha pili kilianza kwa Kasi ambapo Stellenbosch walianza kulisaka lango la Simba SC kwakupiga mipira mirefu iliyoshindwa kuleta manufaa yoyote na kufanya Simba SC waendelee kupata matumaini ya kuendelea pale walipoishia.


Hata hivyo Simba SC kwa mara ya mwisho ilitinga hatua ya fainali mwaka 1993 dhidi ya stella club d'adjame ya Ivory coast na kushindwa kuchukua kikombe hicho.

Simba atakutana na Rs berkane ya Morocco ambao ni washindi mara mbili wa kombe la shirikisho Afrika na mshindi mara wa caf super cup ambapo mchezo wa kwanza utakuwa mei 17,2025 na Simba SC watakuwa ugenini .


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad