Mara baada ya kushinda kesi yake iliyokuwa kamati ya maadili ya TFF, afisa habari wa klabu ya Simba Sc Ahmed Ally ametoa taarifa nzito ya kijembe na kejeli kwa watani wake wa jadi Yanga Sc ambao ndio waliokuwa wamemshtaki siku kadhaa zilizopita.
Ahmed Ally alishtakiwa na Yanga Sc kutokana na taarifa aliyowahi kuitoa iliyokuwa inaeleza kwamba Yanga Sc na Singida Black Stars wameungana ili kuwabana Simba Sc na kuwaondoa kwenye mbio za ubingwa msimu huu.
Taarifa ya hukumu iliyotolewa na TFF siku ya leo Jumamosi tarehe 19 Aprili, zinaeleza kwamba Ahmed Ally hana hatia yoyote dhidi ya shtaka lililopelekwa na Yanga Sc katika kamati ya maadili na hivyo basi yuko huru kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
Taarifa hii imekuwa njema kwa Ahmed Ally ambapo ameibuka na kueleza kwamba ameshinda kesi yake dhidi ya Yanga Sc na kama hawaamini kilichotokea hapa basi waende wakatengeneze kesi mpya.
Ahmed Ally ameendelea kueleza kwamba Yanga Sc hawamuwezi kwa namna yoyote ile haswa kwenye masuala ya kesi za aina hii hivyo basi wanapaswa kubadili upepo huu wa kuendelea kufunguliana kesi ambazo hazina maana wala uhalisia wa aina yoyote.
Yanga Sc wamegonga mwamba kwenye kesi hii na sasa kama wanania ya kutaka kumuumiza Ahmed Ally basi wanapaswa kutengeneza mazingira ya kesi nyingine ambayo itakuwa na mashiko tofauti na hii ambayo imegonga mwamba mara baada ya Ahmed Ally kutoa utetezi wake ambao umempa nafasi ya kuwashinda Yanga Sc.
Yanga Sc watakuwa wameumizwa na hukumu hii kwa sababu pengine walikuwa wanaamini kwamba Ahmed Ally atakutwa na hatia atapewa adhabu kali kama ilivyokua kwa Alikamwe ambaye atalazimika kulipa faini ya milioni 5 kutokana na kosa la kimaadili alilofanya wiki kadhaa zilizopita.