Yanga imerejea katika usukani wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kishindo baada ya kuifunga Timu ya KenGold kwa Magoli 6-1 kwenye Uwanja wa KMC, hivyo kuongoza msimao wa Ligi kwa kufikisha alama 45
Magoli ya #Yanga yamefungwa na Prince Dube dakika ya 1 na 46, Clement Mzize (5 na 42), Pacome Zouzoua (38) na Duke Abuya (85) wakati lile la #KenGoldFC mfungaji ni Selemani Bwenzi (86) aliyefunga kwa kupiga shuti kutoka katikati ya uwanja
Yanga imecheza michezo 17 imeishusha Simba yenye alama 43 ikiwa na michezo 16, wakati KenGold imebaki mkiani ikiwa na alama 6 katika michezo 17