BREAKING: Simba wamepiga chini ofa ya pili kutoka MC Alger
Baada ya jana Simba kukataa ofa ya kwanza ya $350,000 (Tsh 890,322,650) kutoka MC Alger,leo klabu hiyo ya Algeria imetuma ofa ya pili $450,000 (tsh 1,144,700,550) ili kuinasa saini ya Kibu Denis.
Jibu la Simba limebaki pale pale kuwa “Kibu D hauzwi”
MC wana-push sana kumpata nyota huyo kabla ya saa 11 jioni.
Kocha wa MC Alger,Khaled Ben Yahia, anamtaka Kibu ila kuna ugumu kwani Simba hawajataja kiasi gani kinahitajika ili kumuachia Kibu.
Ikumbukwenye Kibu amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na nusu Msimbazi wenye kipengele cha kuondoka endapo $1m italipwa.
Fadlu ni shabiki mkubwa wa Kibu hivyo hatamani nyota huyo kuondoka kati kati ya msimu