SIMBA inaianza safari ya michuano ya Kombe la Shirikisho ikiwa nyumbani kuikaribisha Kilimanjaro Wonders, huku kocha msaidizi wa timu hiyo, Seleman Matola akisema hawatawadharau wapinzani wao hao kwa vile msimu huu, Wekundu wa Msimbazi hawaachi kitu katika mbio za kurejesha mataji klabuni.
Wekundu hao wenye mzuka baada ya kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ikiongoza kundi itaikaribisha timu hiyo ya Kilimanjaro katika mechi ya 64 Bora leo Jumapili kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge, Dar es Salaam.
Mchezo wa leo unatazamiwa kwa umakini zaidi na timu zote mbili huku kila moja ikiwa na hesabu, Simba ikiuchukulia mpambano huo kwa umakini mkubwa ili kuepuka kurudia makosa ya nyuma kwani imewahi kuondolewa mapema na timu za madaraja ya chini katika misimu miwili tofauti nyuma