Rafiki yetu Elie Mpanzu tunaendelea kumpa muda, lakini anapaswa kujitazama kwa kiasi kikubwa. Juzi alifanya jambo moja muhimu la pasi ya kisigino kwa Kibu aliyefunga kwa shuti kali, lakini achilia mbali tukio hilo Mpanzu ambaye tulikuwa tunamsikia ni tofauti na ambaye tulikuwa tunamuona uwanjani juzi.
Mpanzu alikosa mabao ya wazi na wala hakuwa na uamuzi mzuri kama ambavyo tulitegemea kutoka kwake wakati tukisubiri ajiunge na Simba katika dirisha dogo. Anashindwa kuleta tofauti ambayo tunaitegemea kutoka kwake.
Anahitaji kubadilika kwa sababu muda si mrefu mashabiki watamgeuka na kumpotezea uwezo wake wa kujiamini kabisa. Kuna dhana kwamba hakucheza mpira kwa muda mrefu, lakini unapowaza ndani ya kiwango hiki alienda kufanya majaribio na Genk basi ilikuwa wazi kwamba angefeli majaribio.” — Edo Kumwembe.