Wikendi iliyopita Yanga ilishindwa kufuzu robo fainali. Kushindwa kufuzu robo fainali, kumemfanya kiungo fundi wa timu hiyo, Pacome Zouzoua na Nahodha msaidizi, Dickson Job kutoa kauli za matumaini mapya kuwa hawatakubali tena kuona wanawaumiza mashabiki wao tena hivyo wameamua kurudi kivingine kuhakikisha wanatetea makombe yao.
.
“Kuna wakati unaona ni kama ndoto kukosa kucheza robo fainali, kuna wakati unapata matokeo ambayo yanashtua, hii imewaumiza sana mashabiki wetu na hata sisi wachezaji,” alisema Pacome na kuongeza; “Haitakuwa nzuri kama tutawaumiza na kukosa makombe ya ndani ambayo tunayashikilia, tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunatetea makombe yetu yote.”
.
Nahodha msaidizi wa kikosi hicho, Dickson Job alisema “Ujue ligi ni ngumu lakini tuna kikosi cha kuhakikisha tunafanya vizuri, kitu kitakachotusaidia ni kwamba tunataka kila mchezo uwe kama fainali kwetu mpaka tufanikiwe.”