Edo Kumwembe " Chama Angeanza Mechi Aziz K Ana Matatizo"




Wakati wa mapumziko akaingia Pacome. Nilipouliza watu wangu wa karibu ni kwa nini Pacome hakuanzishwa nikaambiwa alikuwa mgonjwa na hakufanya mazoezi kwa siku mbili kabla ya pambano hilo. Ni kweli, naye hakuwa na madhara makubwa. Vipi kuhusu Chama? Kwa nini hakuanzishwa kwa ajili ya kuongeza ubunifu? Ngumu kujua.

Chama hata kama hayupo katika ubora wake ana ubunifu mkubwa katika eneo la mwisho kuliko mchezaji mwingine yeyote nchini. Ramovic angeweza kuwekeza katika hitaji la ubunifu tu katika eneo la mwisho. Ni kitu ambacho Chama hawezi kukuangusha hata kama hana kasi kubwa uwanjani.

Aziz Ki ni mchezaji wa matukio. Anajitokeza zaidi katika kupiga mashuti, kona, penalti, lakini tangu aje Yanga ameshindwa kuitawala mechi kwa kuunganisha safu ya kiungo na ya ushambuliaji. Yeye mwenyewe anahitaji zaidi kufunga kuliko kuunganisha timu. Alikuwa na mechi mbovu na zaidi ana tatizo la kupoteza mipira.”

— Legend Edo Kumwembe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad