Ahmed Ally Kuilipa Yanga Mabilioni, Kisa Kizima Hichi Hapa

Ahmed Ally Kuilipa Yanga Mabilioni, Kisa Kizima Hichi Hapa


Klabu ya Yanga imemtaka Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, kutoka hadharani na kuomba radhi kwa kauli zinazodaiwa kuichafua klabu yao pia wanadai fidia ya Tsh Bilioni 10

Meneja habari huyo alinukuliwa kwakutoa kauli hii;

“Pacome amemaliza mkataba tukiona anafaa tutahangaika nae, Pacome amemaliza mkataba ndani ya Yanga na hana mpango wa kuongeza, mtanyoa ndevu mwaka huu hana mpango wa kuongeza amechoka kuchomwa sindano kila siku kama anazuia mimba”

“Tunaangalia kiwango chake kama kitaturidhisha tutahangaika nae lakini kama ataendelea na mwenendo wake anaoendelea nao tutawaachia…kama tulivyowaachia Chama na tunataja majina ‘Live’ hakuna kutumia code”

Barua hiyo kutoka Yanga imeeleza kuwa kauli hizo ni za upotoshaji na zenye dharau, hivyo imeharibu mahusiano ya klabu na wadau wake kibiashara pamoja na wadhamini.

Yanga wanamtaka Ahmed afanye yafuatayo ndani ya siku tano (5)

1.Kuomba radhi kwa njia sawa na aliyotumia kutoa kauli yake.

2.Kufidia malipo ya Tsh Bilioni 10 za kitanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad