Haji Manara amewatolea uvivu wale waliokuwa wanamsema beki wa Yanga SC na Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Dickson Job kuwa ufupi wake ndio ulikuwa tatizo kwenye safu ya ulinzi ya Stars.
“Tuliambiwa wewe ni kijeba sana kucheza Central Defender, tukaambiwa ufupi wako ndio tatizo kuu kwenye safu ya ulinzi ya timu ya Taifa.
“Sijui kama kuna maswali tena kuhusu ubora wako, ilihali upo vilevile na haujaongezeka urefu hata sentimita moja.
“Top Top performance wewe na miamba wenzio pale nyuma, mechi mbili mfululizo hamjaruhusu hata goli moja mkiwazuia mastrikers warefu kama unju kwa umahiri mkubwa.
“Dickson Job muda mwingine maisha hayapo sawa bado cheki bob wa kiluguru unacheza Afrika, Maguare anazima Old Trafford.” Ameandika Haji Manara kwenye Instagram yake.