Rais Samia Anunua Tiketi 20,000 Kwa Mashabiki wa Taifa Stars Leo Kwa Mkapa
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt @samia_suluhu_hassan amelipia tiketi 20,000 ili mashabiki wa Taifa Stars waingie katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuishangilia timu yao itakapocheza na Dr Congo katika mchezo muhimu wa marudiano wa kufuzu AFCON 2025.
Akitoa taarifa hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamadunia Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amewaomba mashabiki wa Stars wajitokeze kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mgeni rasmi katika mchezo huo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa @kassim_m_majaliwa .
Mchezo utaanza majira ya saa 10:00 jioni
Huku akisisitiza #GoliLaMama liko pale pale.