Klabu ya AmaZulu Fc ya Afrika Kusini imethibitisha kuachana na aliyekuwa kocha wa Simba Sc, Pablo Franco Martin na Msaidizi Aitor Van Den Brule kutokana na mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo ambayo imepoteza mechi zote tatu za kwanza za Ligi Kuu ya Afrika Kusini msimu huum
Taarifa ya klabu hiyo imesema “Tungependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani zetu kwa Pablo Franco Martin na Aitor Van Den Brule kwa mchango wao katika kipindi cha miezi 15 iliyopita katika usukani wa timu.
Kujitolea kwao na bidii yao kumeonekana, na tunathamini juhudi zote ambazo wameweka katika majukumu yao.”
“Tunawatakia kila la kheri katika juhudi zao za siku za usoni na kutoa salamu zetu za dhati wanaposonga mbele katika taaluma zao.”