MCOLOMBIA AMPIGIA SALUTI AFANDE BACCA

MCOLOMBIA AMPIGIA SALUTI AFANDE BACCA


KITASA wa Azam FC Fuentes Mendosa ameshindwa kujizuia na kukiri kuwa Ibrahim Hamad ‘Bacca’ anayekipiga Yanga alistahili kuwa beki bora wa msimu uliopita kutokana na aina ya uchezaji wake ambao umekuwa ukimvutia.

Bacca anashikilia tuzo ya Mchezaji Bora wa Zanzibar na Beki Bora wa Ligi Kuu Bara msimu ulioisha, ametajwa na Mendosa kuwa anavutiwa na aina ya uchezaji wake akimtaja kuwa ni beki ambaye anacheza kwa kujiamini, hafanyi makosa wala hamhofii mpinzani.

“Simfahamu jina lakini anacheza Yanga anavaa jezi namba (4) ni mchezaji ambaye navutiwa na aina ya uchezaji wake na nilipoambiwa amepewa tuzo ya mchezaji bora wa msimu nimejisikia faraja kwani jicho langu limekuwa likimtazama sana,” amesema.

“Ni mchezaji ambaye anafika maeneo muhimu kwa nafasi. Hafanyi makosa, hapitiki kirahisi, nafurahishwa na aina yake ya uchezaji. Kuna vitu navichukua na naamini kama ikitokea nikapata nafasi ya kuzungumza na mchezaji huyo kuna mambo mazuri natamani kumuelekeza ili aendelee kuwa imara.”

Mendosa akizungumzia msimu uliopita, amesema ulikuwa ni bora kwake kwa sababu alikuwa mgeni kwenye ligi, lakini aliingia kwenye mfumo haraka na kufanya kazi nzuri ambayo iliibua ushindani kati yangu na walionitangulia.

“Mwanzo wangu bora ndani ya muda mchache niliocheza ndani ya Azam FC matarajio ni kupambana kuwa na mwendelezo lengo ni kuona napata nafasi ya kufanya kile kinachotarajiwa na viongozi walionipa nafasi ya kuwatumikia, lakini pia kujiweka kwenye nafasi ya kutoa ushindani kwa wapinzani,” amesema na kuongeza:

“Nimekuja Tanzania kufanya kazi na kilichonileta ni mpira acha niutumikie na nina kila sababu ya kuwa mchezaji aliyeipa Azam mafanikio kwani niliwaaminisha naweza kucheza na waliamini hilo kwa kunipa nafasi nitahakikisha naipa mataji timu hii.”

Medosa hadi sasa ameitumikia Azam FC kwa miezi sita tu baada ya kusajiliwa dirisha dogo msimu ulioisha ameliambia Mwanaspoti kuwa lengo lake ni kuipa Azam FC mataji na kuipeleka hatua nzuri kiushindani ndani na nje.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad