Gamondi Awaonya Mastaa wake

 

Gamondi Awaonya Mastaa wake

Licha ya kikosi chake kuonyesha ubora mkubwa katika mechi za mwanzo msimu huu, Kocha Mkuu wa Yanga Sc Miguel Gamondi amesema haimaanishi kama wako salama na itakuwa rahisi kwao kupata mafanikio kama ilivyokuwa msimu uliopita.


Gamondi amesema msimu huu anatarajia kupata upinzani mkali zaidi kutoka kwa wapinzani wao katika michuano yote wanayoshiriki kwani kila timu inajiandaa kwa lengo la kushindana na Yanga Sc.


"Kila timu sasa inataka kuifunga Yanga Sc, inabidi tupambane, tusijidangaye kuwa tupo kwenye mstari salama, ninawaambia haya hata wachezaji wangu, wanatakiwa kila siku waongeze juhudi na mazoezi zaidi ili tuwe bora kila kukicha kwani wenzetu nao wanaongeza ubora ili watufikie au watupite."


Nini Maoni Yako Mdau wa Soka?

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad