Simba Yathibitisha Kuachana na Manula, Jobe, Onana, Kanoute, Babacar

 

Simba Yathibitisha Kuachana na Manula, Jobe, Onana, Kanoute, Babacar

Klabu ya Simba itaendelea kuachana na wachezaji wake wa msimu ulioisha , muendelezo wa “Thank You” unaendelea Lunyasi.


Kwa mujibu wa Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema Sadio Kanoutè, Babacar Sarr , Willy Onana , Pa Omar Jobe ni miongoni mwa nyota hao ambao huenda wasiwe sehemu ya kikosi hicho msimu ujao baada ya kuachwa kwenye kikosi kilichoelekea nchini Misri kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao.


“Hawa mliowaona hapa ndiyo wachezaji wa Simba kwa msimu ujao 2024/25. Taarifa ya wachezaji ambao hamjawaona hapa itatoka baadaye muwe na subira.


“Hawa ni Pa Omar Jobe, Babacar Sarr, Sadio Kanoute, Aishi Manula, Willy Esomba Onana, wote hawa bado ni wachezaji wa Simba kwa sababu wa mikataba na Simba lakini je, wataendelea kusalia Simba msimu ujao?


“Endeleeni kutupa subira kidogo hapo, taratibu za ndani zikamilike, tutakuja kuwajulisha ni maamuzi gani yamefanyika kwa watu wote hawa ambao hamjawaona hapa leo,” Ahmed.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.