Mshambuliaji mpya wa Yanga, Prince Dube amejiunga rasmi na kambi ya timu hiyo na kuanza mazoezi mara moja na wenzake huku ikiwa ni siku yake ya kwanza kazini katika kikosi hicho cha mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC.
Dube raia wa Zimbabwe amejiunga na Yanga msimu huu akitokea Azam Fc ambako amedumu kwa miaka kadhaa kabla ya kuomba kuvunja mkataba na kutua Jangwani.
Wachezaji wa Yanga wameanza kuripoti kambini Avic Town Kigamboni leo Julai 8, 2024 ikiwa ni mwanzo wa maandalizi ya msimu mpya kueleka msimu ujao 2024/25.