BREAKING: Simba Wamtambulisha Kocha Mpya Fadlu Davids

 

Simba wamtambulisha Kocha Mpya Fadlu Davids

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wamemtambulisha kocha Mkuu Fadlu Davids, Raia wa Afrika Kusini.


Kocha huyo ambaye alikuwa kocha msaidizi Raja Casablanca, anakwenda kuchukuwa jukumu la Kocha Mkuu Simba SC baada ya Wekundu hao wa Msimbazi kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu Benchikha katikati mwa msimu uliopita.


Baada ya kuachana na Benchikha ambaye aliaga kwa kusema anakwenda kushughulikia kile alichokiita matatizo ya kifamilia, timu iliongozwa na Kocha Juma Mgunda kama Kocha Mkuu wa muda akishirikiana na Msaidizi wake Selemani Matola.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad