Ofisa Habari Yanga SC, Ally Kamwe amesema kuwa usajili wanaoufanya watani zao wa jadi, Simba Sc ni za kawaida hivyo wategemee mateso tena msimu ujao.
Simba wametambulisha wachezaji watatu ambao ni Joshua Mutale kutoka Power Dynamos ya Zambia, Lameck Lawi kutoka Coastal Union ya Tanga na Steven Mukwala raia wa Uganda akitokea Asante Kotoko ya Ghana.
“Kosa kubwa mnalofanya ni kulinganisha sajili za yanga na wachezaji wengine, mnawapa presha wachezaji wadogo wadogo. Chama yupo kwenye top 20 ya wachezaji bora wa muda wote wa CAF. Huyu Joshua wa Simba sio mchezaji mbaya ila ni aina ya wachezaji ambao tulikuwa nao miaka mine iloiyopita.
“Sidney Urikob, Patrick Sibomana, Juma balinya ni aina ya wachezaji ambao tulikuwa nao miaka mine iliyopita. Zambia ina mwamba mmoja tu, pamoja na straika kennedy Musonda wachezaji wengine ni wa shirikisho ambao ukienda nao hatua ya awali mtawasha moto uwanjani mtafukuzwa.
“Sisi tumetambulisha mtu mmoja tu nchi nzima imetetemeka kwa sababu huyo mtu ni mwamba,” amesema Kamwe.