Shaffih Dauda 'Tatizo la SIMBA ni MO Dewji Anataka Kuwa Mmiliki wa Timu'

Shaffih Dauda 'Tatizo la SIMBA ni MO Dewji Anataka Kuwa Mmiliki wa Timu'

 Tatizo la Simba kwa miaka yote ni MOHAMMED DEWJI ‘MO’ mwenyewe.

Wakati watu wengi wanajiuliza tatizo la Simba ni nini? Jibu ni jepesi sana, tatizo kubwa la Simba ni Mohammed Dewji ‘Mo’! Lengo kubwa la huyu bwana ni kutaka kuwa mmiliko wa Simba na mara kadhaa ameshajitangaza hivyo.


Habari ya kuwa mwekezaji wa Simba kwa 49% hataki kabisa kuisikia, anatengeneza mazingira ya kuipiga ‘shot’ Simba hadi lengo lake la kuimiliki klabu litimie.


Ifike wakati Mo akubali kuwa mwekezaji wa Simba au kama vipi akaanzishe timu au anunue timu ili atimize lengo lake la kuwa mmiliki wa klabu.


Anaposema kuna watu wanamkwamisha anamaanisha wanamkwamisha kuimiliki Simba sio kuwekeza. Kama ni kuwekeza mchakato ungekuwa umeshakamilika miaka mingi nyuma lakini yeye anataka kuwa mmiliki zaidi ya 51%


Hata uendeshaji wa timu ni wa kienyeji tangu mwaka 2018 huku yeye akiwa kama mmiliki na hujitambulisha hivyo kote duniani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.