Timu ya Simba Wakijisahau tu, Mzamiru Anasepa

 

Timu ya Simba Wakijisahau tu, Mzamiru Anasepa

Wakati Simba ikiwa kwenye mapambano ya kuhakikisha Kibu Denis anasaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Msimbazi, kuna tetesi kuwa Mzamiru Yassin yupo kwenye mawindo ya Ihefu na Azam FC.


Inatajwa kuwa tayari Ihefu imewasilisha ofa mezani kwa Mzamiru huku Azam FC ikiwa imeonesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo ambaye amedumu Simba kwa muda mrefu tangu aliposajiliwa akitokea Mtibwa Sugar.


Mkataba wa Mzamiru na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu lakini hadi sasa bado hajaongeza mkataba mwingine, kwa hiyo kama Simba haitamuongezea mkataba mpya huenda akaondoka akiwa mchezaji huru.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.