Azam Vs Simba ni Kivumbi Leo, Wanagombani Nafasi ya Pili Kushiriki Ligi ya Mabingwa

Azam Vs Simba ni Kivumbi Leo, Wanagombani Nafasi ya Pili Kushiriki Ligi ya Mabingwa
Azam Vs Simba Leo


Azam Vs Simba ni Kivumbi Leo, Wanagombani Nafasi ya Pili Kushiriki Ligi ya Mabingwa


AZAM V/s SIMBA [Mzizima Derby] ndio mechi kubwa kwa siku ya leo kwenye Ligi ya NBC. Ni mechi ya timu ambazo kimahesabu bado zina nafasi ya kuwa mabingwa kwa sababu bado zinaweza kufikia alama za Yanga.

Kwa uhalisia Azam na Simba nafasi yao ni ndogo sana kushinda ubingwa msimu huu, kilichobaki kwao ni kupigania nafasi ya pili ili msimu ujao kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika.

Azam ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 57 baada ya kucheza michezo 25, Simba ipo nafasi ya tatu na alama zake 53 baada ya kucheza michezo 24 [Azam ipo mbele ya Simba kwa mchezo mmoja].

Simba ipo nyuma ya Azam kwa alama nne [4], hata kama leo itashinda bado itabaki nafasi ya tatu [3] kwenye msimamo huku tofauti yao ikiwa ni alama moja [1]. Kama Azam itashinda itaongeza tofauti ya alama dhidi ya Simba na kufikia alama saba [7].

Ni mechi nzuri kuitazama kwa kuwa kila timu inahitaji alama tatu, endapo Azam itashinda itafikisha alama 60 lakini Simba ikishinda itafikisha alama 56. Matokeo ya sare yataifanya kila timu kuongeza alama moja ambapo Azam itafikisha alama 58 na Simba itafikisha alama 54.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.