Ahmed Ally: Kuwatoa Al Ahly Robo Fainali Wala Sio Kazi kubwa

 

Ahmed Ally: Kuwatoa Al Ahly Robo Fainali Wala Sio Kazi kubwa

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kuitoa Klabu ya Al Ahly kwenye michuano ya CAFCL sio jambo kubwa kwa Simba.


Ahmed amesema hayo kuelekea mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba watakipiga na Ahly mnamo Machi 29, 2024 katika Dimba la Mkapa.


"Kuitoa Al Ahly kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika haitakuwa ajabu, Simba tumeshafanya maajabu makubwa kwenye bara la Afrika! Kwa hiyo kuwatoa Al Ahly sio kitu ambacho kinatushinda, tunahitaji muda mzuri, utulivu mkubwa na kufanya maandalizi.


"Na maandalizi bab-kubwa ambayo tumeyakusudia, kikosi chetu kinatarajia kuondoka kesho kwenda Zanzibar kuweka kambi ya siku saba hadi nane ili kumpa kocha muda wa kutosha kuandaa timu ya kuwatoa Al Ahly.


"Tunaenda Zanzibar kwa sababu tutapata utulivu, tunahitaji kuwa na program ya mazoezi majira ya usiku na Zanzibar kuna miundombinu ya kutosha kwa ajili ya timu yetu kufanya mazoezi usiku muda ambao mechi yetu na Al Ahly itachezwa," amesema Ahmed Ally.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.