Hawa Hapa Washindi wa Tuzo za CAF 2023

Hawa Hapa Washindi wa Tuzo za CAF 2023


Mchezaji wa Al Ahly ya Misri Percy Tau ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa Mwaka wa CAF 2023 kwa Wachezaji wa ndani ya Afrika akiwashinda Fiston Mayele wa Yanga/Pyramids na Peter Shalule wa Mamelod Sundowns.


Wengine waliochukua tuzo ni Golikipa wa Al Hilal ya Saudi Arabia na Timu ya Taifa ya Morocco Yassine Bounou ambaye ameshinda tuzo ya golikipa bora wa mwaka wa CAF akiwashinda Andre Onana wa Man United na Cameroon pamoja na Mohammed El Shenawy wa Al Ahly ya Misri na Timu ya Taifa ya Misri.


Kocha wa Timu ya Taifa ya Morocco Walid Regragui ameshinda tuzo ya Kocha bora wa Afrika wa mwaka 2023 wa CAF akiwashinda Kocha wa Simba SC/USM Alger Adelhak Benchikha na Aliou Cisse wa Timu ya Taifa ya Senegal .


Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Nigeria na Klabu ya Napoli ya Italia Victor Osimhen ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa mwaka wa CAF akiwashinda Mohammed Salah wa Misri/Liverpool na Achraf Hakimi wa PSG/Morocco.


2023 CAF Awards Winners List

Men's Player of the Year: Victor Osimhen (Napoli and Nigeria)

Women's Player of the Year: Asisat Oshoala (Barcelona and Nigeria)

Men's Coach of the Year: Walid Regragui (Morocco)

Women's Coach of the Year: Desiree Ellis (South Africa)

Men's National Team of the Year: Morocco

Women's National Team of the Year: Nigeria

Men's Goalkeeper of the Year: Yassine Bounou (Al-Hilal and Morocco)

Women's Goalkeeper of the Year: Chiamaka Nnadozie (Paris FC and Nigeria)

Men's Young Player of the Year: Lamine Camara (Metz and Senegal)

Women's Young Player of the Year: Nesryne El Chad (Lille and Morocco)

Men's Club of the Year: Al Ahly (Egypt)

Women's Club of the Year: Mamelodi Sundowns (South Africa)

Men's Interclub Player of the Year: Percy Tau (Al Ahly and South Africa)

Women's Interclub Player of the Year: Fatima Tagnaout (AS FAR and Morocco)


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.