Bao la Kibabage, Yanga yamshtaki mwamuzi CAF

 

Bao la Kibabage, Yanga yamshtaki mwamuzi CAFBaada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Medeama, uongozi wa klabu ya Yanga umeliandikia barua Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kulalamikia uamuzi mbaya ulioonyeshwa na mwamuzi aliyechezesha mchezo wao huo.


Yanga ilikuwa ugenini kwenye mchezo huo uliochezeshwa na Ibrahim Mutaz ambaye alikuwa katikati, na kusaidiwa na Attia Amsaad kutoka Libya na Khalil Khasan kutoka Tunisia.


Akizungumza nasi, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Rodgers Gumbo alikiri kuandika barua ya malalamiko kwa CAF wakimlalamikia mwamuzi (Mutaz) kwa kuonyesha upendeleo kwenye mchezo wetu dhidi ya Medeama


“Ni kweli tumepeleka barua ya malalamiko kwa CAF kutokana na kuwa na ushahidi wa matukio ambayo ni wazi hatukutendewa haki ambayo ni pamoja na rafu ambayo mchezaji wetu Nickson Kibabge alichezewa na mchezaji wa Medeama ambaye alistahili kuonyeshwa kadi nyekundu lakini refa hakufanya hivyo.


“Lakini pia kuna tukio la bao letu halali ambalo Kibabage alifunga lakini refa akalikataa akiwaaminisha watazamaji na wachezaji kuwa waliotea hivyo sio bao sahihi lakini baada ya kulitazama tumebaini uonevu; 


“Tumewaandikia ili wajue nini cha kufanya kwa sababu matukio kama yale yananyima timu haki ya kupata ushindi na kuipa nyingine matokeo ambayo haijastahili,” alisema Gumbo.


Tukio la rafu dhidi ya Kibabage linalolalamikiwa na Yanga ni lile la dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza ambapo beki Kwadwo Amoako alimrukia kwa miguu miwili nyota huyo wa Yanga ambapo kwa mujibu wa sheria ya faulo na utovu wa nidhamu, adhabu yake ni kadi nyekundu ya moja kwa moja ingawa refa Mutaz alionyesha kadi ya njano.


Lakini pia, bao la Kibabage lilikataliwa kimakosa kwa kile kilichodaiwa kuwa aliotea kabla ya kufunga wakati hakuwa ameotea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.