Amri Kiemba: Mchezaji Chama Asishindanishwe na Pacome


Chama na Pacome
Chama na Pacome

LEGEND. @amrikiembatz ameandika

Hivi karibuni kumekuwa na mijadala kadhaa mitandaoni kuhusiana na Wachezaji Clatous Chama wa Simba SC na Pacome Zouzoua wa Yanga, wengi wanabishana na kutaka kujua nani bora zaidi ya mwenzake.

Mashabiki wengine wakienda mbali zaidi na hata kuniuliza, kama mimi ningekuwa Kocha na niko nao wote kikosini nitaanza na mchezaji gani kati ya hao wawili.

Kwangu mimi binafsi huu ni mjadala wenye tija kwa ambao wameamua kujadili hili, mimi sioni kama hawa ni wachezaji wa aina moja kuwalinganisha, nadhani unaweza kuwashindanisha Wachezaji kutokana na nafasi wanayocheza lakini hawafanani kwa maana ya utekelezaji wao wa majukumu.

Chama ni aina ya Wachezaji ambao kwenye soka la sasa hivi wanaanza kupotea kwa maana wale wachezaji ambao walikuwa wanacheza huru timu inapokuwa na mpira, hawa ni Wachezaji wanaoanza kupotea kwenye uchezaji wa sasa.

Wakati Pacome ni mchezaji wa kisasa ambaye anaweza kufanya majukumu yote mawili kwa wakati mmoja, anaweza kuchezesha timu na anaweza kukusaidia timu kuweza kupata matokeo na anaweza kukusaidia kujilinda kama namba sita, Pacome anabadilika kutokana na eneo na vipindi.

Kipindi ambacho timu ina mpira Pacome anaweza kuwa namba 6, 8 na anaweza kuwa namba 10, wakati timu haina mpira Pacome anaweza kuwa namba 6 halisi akazuia kama ambavyo namba 6 anafanya na pia anaweza kuwa namba 8 wa kisasa.

Ukitaka kuchagua nani zaidi itabidi uchague kipengele ambacho wote wanakifanya vizuri ambacho ni uimara wao, usichukue udhaifu wa mmoja na kulinganisha, kwangu mimi kila mmoja ana ubora wake kulingana na eneo lake ambalo yuko bora zaidi.

Pacome anaweza kumshinda Chama kwenye vitu vingi ndani ya kiwanja kimbinu kwa sababu anaendana na mchezo wa kisasa lakini Chama linapokuja suala la timu ina mpira na anatakiwa kufanya ubunifu, basi amekuwa akifanya kwa asilimia zaidi ya 80 isipokuwa kwenye kujilinda labda anatumia asilimia 20 kushuka chini, wakati Pacome anafanya kwa ubora ule ule, tukisema nani ni bora tutafute mchezaji ambaye wanaendana sifa na kuweza kupata mchezaji bora ila mimi naona wote wazuri.

Kwako limekaaje kama mdau wa mpira wa miguu ____?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.