Uongozi wa Yanga Watamba, Yanga Kufika Mbali Kuliko Timu Yoyote Bongo
Kwa muda mrefu mashindano ya Afrika [CAF Champions League na CAF Confederation Cup] yamekuwa yakitawaliwa na timu za Kaskazini mwa Afrika.
Yanga kukutana na timu mbili kwenye hatua ya makundi kutoka ukanda wa Kaskazini mwa Afrika [Al Ahly na CR Belouizdad] inatupa fursa ya kucheza na timu zenye uzoefu na endapo tutatoka kwenye kundi hilo tutakuwa tumepata mechi zenye ushindani mkubwa.
Kwa ubora wa kikosi chetu, tunaamini tutavuka hatua ya makundi na kwenda hatua inayofuata [Robo Fainali] na safari yetu itaendelea hadi hatua ambayo hakuna timu ya Tanzania iliyowahi kufika kwenye mashindano haya ya Ligi ya mabingwa Afrika.