Kocha Geita Gold atakiwa kujisalimisha kwa Mkurugenzi



Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Zahara Michuzi amemtaka kocha mkuu wa timu ya Geita Gold inayomilikiwa na halmashauri hiyo afike ofisini kwake mara moja kueleza kiini cha matokeo mabaya.


Zahara ametoa maelekezo hayo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari mjini Geita na kueleza haridhishwi na mwenendo wa timu hivo benchi la ufundi wafike kumueleza kikwazo ni nini.


Geita Gold Fc inafundishwa na kocha Hemed Suleiman, ambaye tangu apewe dhamana hiyo, imecheza michezo nane ya ligi kuu ya Tanzania bara na kupoteza michezo minne, kupata sare tatu na ushindi mmoja pekee.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad