Edo Kumwembe Amkingia Kifua Manula Simba

Edo Kumwembe Amkingia Kifua Manula SimbaMchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini, Edo Kumwembe amemtetea kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula kutokana na kipigo cha bao 5-1 walichokipata kutoka kwa watani zao Yanga, Jumapili iliyopita Novemba 5, 2023 katika Dimba la Mkapa.


Edo amesema kuwa ametazama mchezo huo hakuna kosa lolote lililofanywa na Manula na likasababisha bao kama ambavyo baadhi ya watu wanasema.


"Aishi? Hapana. Naam, nimetazama mabao yote manne ya Yanga yaliyofungwa katika open play, sijaona kosa la Aishi.


"Nitatoa mfano. Kuna bao ambalo kipa anafungwa mnarudisha mpira kati, halafu kuna bao ambalo anacheza huwa Waingereza wanaita Extra ordinary save yaani save isiyo ya kawaida, save ya kiajabu.


"Kama Aishi angepangua kichwa cha Musonda ingekuwa Extra Ordinary save. Ni kama Onana alivyompangulia Haaland siku ile. Lakini kama unafungwa unaweka tu na hakuna lawama. Kama Haaland alivyofunga baadae. Tatizo lilikuwa kukariri.


"Tunajua kwamba mtu akikaa nje muda mrefu hawi wa moto. So kwa sababu Aishi alikaa nje kwa muda mrefu tumekariri kwamba alifungwa kizembe mabao yote bila ya kuchambua mabao yenyewe.


"Kama angedaka Ally akafungwa mabao matano wangesema 'Aishi si kasharudi kwa nini asipangwe?' Mpira wetu umejaa lawama," amesema Edo Kumwembe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.