Viingilio Mechi ya Yanga vs Al-Merrikh Hivi Hapa
Viingilio vya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya kikosi chetu cha Yanga SC dhidi ya Al Merrikh unaotarajiwa kuchezwa Septemba 30, mwaka huu, vimewekwa hadharani.
Mchezo huo wa kuwania nafasi ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, utachezwa Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam ambapo mageti yatakuwa wazi kuanzia saa 4:00 Asubuhi.
Viingilio vya mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 1:00 usiku, vimewekwa katika makundi manne ambapo MZUNGUKO ni Tsh. 10,000, V.I.P B Tsh. 20,000, V.I.P A Tsh. 50,000 na ROYAL Tsh. 100000.
Akizungumzia viingilio hivyo, Ofisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe, amesema: “Ukitaka kujua wana Yanga wana ugwadu na huu mchezo, tayari baadhi yao wameshaingia kwenye mfumo kuangalia tiketi, tayari baadhi ya mashabiki wameshanunua tiketi kupitia mfumo kabla ya sisi kutangaza mfumo hadharani.
“Sisi sio klabu namba tatu kwa ubora wa Afrika kwa bahati mbaya, ni lazima tuoneshe hilo kwa kutinga hatua ya makundi. Hivyo hizi tiketi zinaweza kuisha mapema mno kama shabiki hutanunua tiketi mapema.”
Kikosi chetu cha Yanga SC kitaingia katika mchezo huo kikiwa na mtaji wa magoli 2-0, tulioupata ugenini nchini Rwanda, Septemba 16, 2023.
SOMA PIA:
Matokeo Yanga vs Al Merreikh Haya Hapa Leo 30 September 2023