Yanga Hawapoi, Watua Dar Kwa Kishindo, Fasta Waunganisha Safari Singida

Yanga Hawapoi, Watua Dar Kwa Kishindo, Fasta Waunganisha Safari Singida

 Yanga Hawapoi, Watua Dar Kwa Kishindo, Fasta Waunganisha Safari Singida

Kikosi cha Yanga kimewasili salama Alfajiri ya leo Jijini Dar es Salaam kikitokea Afrika Kusini ambako juzi kilikata tiketi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuwatoa wenyeji, Marumo Gallants.


Na baada ya kuwasili Yanga wanaunganisha safari kwenda Singida kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Singida Big Stars Jumapili.


Yanga imeitoa Marumo Gallants ya kwa jumla ya mabao 4-1, ikishinda 2-0 nyumbani na 2-1 ugenini Jumatano na kwenye Fainali itakutana na USM Alger ya Algeria.


Yenyewe USM Alger imeitoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast baada ya sare ya 0-0 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani.


Yanga itaanzia nyumbani katika Fainali ya kwanza Mei 28 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Algeria kwa mchezo wa marudiano Juni 3 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers.


Tayari Yanga wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya pili mfululizo wakiwa wana mechi mbili mkononi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.