TFF kuchunguza upangaji wa matokeo kwenye mechi hizi

Published from Blogger Prime Android App

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeutaarifu umma kuwa limepokea malalamiko ya kimaadili dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora (TAREFA), Yusuph Kitumbo na Kocha Ulimboka Mwakingwe

Malalamiko hayo yanayohusisha madai ya upangaji matokeo yamewasilishwa na klabu ya Ligi ya Championship, Fountain Gate FC na tayari yamewasilishwa katika Kamati ya Maadili ya TFF ili yafanyiwe kazi kwa mujibu wa Kanuni za Maadili za TFF

Ili kulinda hadhi ya mpira wa miguu, TFF inawakumbusha wanafamilia wote wa mpira wa miguu kuwa itachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na upangaji matokeo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.