Kisa Kauli ya Kufa Kiume..Mchambuzi Bongo Awashukia SIMBA "Kila Mwaka Wanaishia Hapo Hapo tu"
Mchambuzi maarufu wa masuala ya soka nchini, Saleh Ally Jembe amesema kuwa Simba SC wanapaswa wabadilishe mawazo na mipango yao ili wajitume na kuhakikisha wanavuka katika hatua ya ya robo fainali ya michuano ya CAF baada ya kuwa wanakomea kwenye hatua hiyo kila mwaka.
Jembe amesema hayo baada ya Simba SC kuondolewa katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Mabingwa Afrika kwa kuondolewa na Wydad Casablanca.
“Tunaweza kuwapongeza Simba SC kwa kucheza vizuri lakini hatuwezi kusema wamekufa kiume. Huwezi kuwa mwanaume kila siku unafia kwenye msingi kabla hujafika nyumbani kwako, kila siku unasema tumekufa kiume.
“Simba kila mwaka wanaishia palepale, ni kweli walikuwa wanacheza na Bingwa mtetezi wa Afrika, ni mechi ngumu lakini ukiangalia mchezo ule walikuwa wameingia kwenye nafasi ya kuvuka.
“Simba wamekuwa wakikosea kila siku, wanakosea nyumbani wakipata nafasi hawaitumii au wanakosea ugenini. Tazama mechi ya Kaizer Chiefs, mechi ya Orlando Pirates hata kwa Wydad walikuwa wanashinda hapa Dar hata bao 3, lakini walipoenda kule baada ya kutolewa wanasema wamekufa kiume.
“Nadhani wanatakiwa wabadilishe mentality ya kufa kiume badala yake wakafie fainali. Haiwezekani wakashinda wakati wanapata kila kitu. Zamani tulisema Yanga wajifunze kwa Simba kimataifa, lakini Yanga kwa nini sasa wamevuka, hapo unaona Simba wanatakiwa wajifunze kwa Yanga,” amesema Jembe