'Yanga kupoteza mechi zilizosalia ni ndoto, ila hatutoki mikono mitupu' - Ahmed Ally Achutama

Ahmed Ally

'Yanga kupoteza mechi zilizosalia ni ndoto, ila hatutoki mikono mitupu' - Ahmed Ally Achutama

Meneja Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa uwezekano wa wapinzani wao Yanga kupoteza mechi tatu zilizosalia za Ligi Kuu Bara ni mdogo sana hivyo wanalazimika kupambana ili kuhakikisha wanabeba ubingwa wa kombe la Shirikisho la Azam.


Ahmed amesema hayo kuelekea mchezo wao wa nusu fainali ya Kombe hilo dhidi ya Azam FC utakaopigwa kesho Jumapili katika dimba la Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.


Kauli hiyo ya Ahmed inakuja ikiwa ni siku chache baada Simba ya kutoa sare dhidi ya Namungo hali iliyofifisha ndoto yao ya kusaka ubingwa wa ligi kuu huku kinara wa ligi hiyo, Yanga akibakisha mchezo mmoja tu atangaze ubingwa.


"Tunahitaji kushinda mchezo wa Nusu Fainali dhidi ya Azam FCili tutimize malengo yetu ya kuchukua ubingwa wa mashindano haya. Haujawa msimu mzuri sana, tumetolewa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini vilevile matumaini yetu kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara hamezidi kufifia sana baada ya sare ya juzi dhidi ya Namungo FC.


"Kwa sasa tuna 20% ya kuwa mabingwa wa Ligi Kuu na 80% kuukosa, lazima tuambiane ukweli. Uwezekano wa Simba kushinda mechi zote tatu ambazo zimesalia upo lakini uwezekano wa mpinzani wetu tunayewania nae ubingwa kupoteza mechi zote tatu hapo ndio kwenye ugumu.


"Kwa hiyo mahali pekee ambako hakuhitaji bahatinasibu kuupata ubingwa wake ni kwenye Azam Sports Federation Cup. Ili tuweze kuchukua ubingwa huu, inatulazimu tucheze vizuri katika mechi mbili [Nusu Fainali na Fainali] tukiweza kufanya hivyo tunachukua ubingwa.


"Hatupo tayari kuona msimu huu tunamaliza patupu kama ambavyo ilikuwa msimu uliopita. Msimu huu tunahitaji kumaliza na jambo, tunahitaji taji. Kombe la Azam Sports Federation Cup haliondoi machungu ya kushindwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wala machungu ya kukosa ubingwa wa Kigi Kuu lakini linaonesha kuna kazi tumeifanya kwenye msimu husika," amesema Ahmed Ally.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad