MO Dewji Amuondoa Mzamini BETWAY Kwenye Jezi yake, Mangungu Aitaki Kabisa Jezi Avaa shati

MO Dewji Amkataa Mzamini BETWAY Kwenye Jezi yake, Mangungu Aitaki Kabisa Jezi

Katika tamasha kubwa la Simba Day lililofanyika jana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, hali ya umati wa mashabiki waliojazana na kuvaa jezi mpya za msimu chini ya mdhamini mkuu Betway ilikuwa ya kuvutia sana. Hata hivyo, jambo lililozua maswali miongoni mwa mashabiki na wachambuzi ni namna viongozi wakuu wa klabu walivyojipambanua katika mavazi yao.


Rais wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji, alionekana akiwa amevalia jezi ya Simba lakini bila nembo ya mdhamini mkuu Betway. Swali linalojitokeza ni je, hii ilikuwa ni kulinda taswira yake binafsi na brand zake nyingine kama Mo Cola, Mo Foundation, au ni suala la imani na misimamo ya kidini?


Ikiwa ni dini, kwa nini brand zake binafsi kama Mo Cola na Jayruty ziliendelea kubaki kwenye jezi ?, Ikiwa ni suala la kulinda brand binafsi, basi ni changamoto kwa sababu viongozi wa klabu kubwa duniani hujitambulisha kwanza na brand ya timu, kisha mambo mengine huja baadaye.


Pia Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu, yeye alichagua kuvaa shati na suruali nadhifu badala ya jezi ya klabu. Kwa mtazamo inaonekana kama vile hakuwa sehemu ya “shangwe za Simba Day” ambazo mashabiki walizama ndani yake.


Kiongozi wa juu anaposhindwa kuonyesha mshikamano na mashabiki wake kwa kuvaa jezi ya timu katika siku kubwa kama hii, inaleta tafsiri nyingi na tofauti kwa mashabiki, Simba ni klabu kubwa yenye wafuasi wengi Katika biashara ya soka, taswira ni kitu cha kwanza kupewa kipaumbele, Wachezaji, viongozi, mashabiki na wadhamini wote wanatakiwa kupeleka ujumbe mmoja.

MO Dewji Amuondoa Mzamini BETWAY Kwenye Jezi yake, Mangungu Aitaki Kabisa Jezi Avaa shati


Pale viongozi wanapojitenga, inaleta tafsiri kwamba bado kuna pengo kubwa kati ya management na fan base. Hii inaweza kumvuruga hata mdhamini mkuu, kwa sababu brand yake haionekani kuungwa mkono na viongozi wa juu.


Viongozi wa juu wanapaswa kutengeneza uwiano wa wazi kati ya brand zao binafsi na brand ya Simba, Hakuna ubaya kuwa na misimamo ya kiimani, lakini kunahitajika mawasiliano ya moja kwa moja


Simba SC kama taasisi, inahitaji kufanya kazi kubwa katika kuhakikisha viongozi wanafuata “club branding strategy” ili kuimarisha taswira ya pamoja mbele ya mashabiki na wadhamini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad