Bingwa wa Kombe la Cecafa Kagame CUP Kuvuna Dola 30,0000

Bingwa wa Kombe la Cecafa Kagame CUP Kuvuna Dola 30,0000



Ni jumla ya Dola za Marekani 60,000 ndizo zitakazotolewa kwa timu tatu bora katika mashindano ya Cecafa Kagame Cup.


Mchezo wa kuwania Medali ya shaba na Dola za Marekani 10,000 utazikutanisha APR FC (Rwanda) na KMC FC ya Ligi Kuu Tanzania Bara, huku timu mbili ambazo hazijawahi kunyanyua taji la kanda kabla ya Al Hilal SC (Sudan) na Singida Black Stars FC (Tanzania) zikipangwa kumenyana katika fainali.


Dola za Marekani 30,000 na Medali za dhahabu vitatolewa kwa Mabingwa, huku mshindi wa pili akitwaa medali ya fedha na dola 20,000.


Timu ya Al Hilal SC iliitoa APR FC kwa mabao 3-1, huku Singida Black Stars FC ikiilaza KMC FC mabao 2-0 katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.


Laurentiu Aureliant Reghecampf, kocha wa Al Hilal SC ameweka wazi kuwa timu yake iko tayari kabisa kufanya kila kitu na kujaribu kushinda kombe hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad