Klabu ya Simba imethibitisha kuwa itacheza na klabu ya Gor Mahia ya Kenya kwenye kilele cha tamasha kubwa la kila mwaka la klabu hiyo almaarufu 𝐒𝐢𝐦𝐛𝐚 𝐃𝐚𝐲 kwa mwaka 𝟐𝟎𝟐𝟓
𝐒𝐢𝐦𝐛𝐚 𝐃𝐚𝐲 𝟐𝟎𝟐𝟓 itafanyika Septemba 10 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ikiwa ni utaratibu wa kila mwaka kwa klabu hiyo kualika timu kutoka nje ya nchi na kucheza nayo mechi ya kirafiki kwenye siku yao ambayo huambatana na utambulisho wa wachezaji wa klabu hiyo.