Yanga wanaamini thamani ya Mzize inazidi kupanda siku hadi siku kutokana na kiwango cha Mzize kwenye michuano ya CHAN.
Kabla ya CHAN kuanza Yanga walikadiria Mzize ana thamani ya $1m ila kutokana na kiwango chake kwa siku za hivi karibuni Yanga wanahisi thamani yake imepanda zaidi na kama ataendelea kukiwasha basi thamani yake itapanda zaidi hadi $2m.
Mauzo ya wachezaji ni biashara kubwa duniani,thamani za wachezaji zinabadilika kila kukicha kutokana na viwango vyao,Yanga pia wanalijua hilo.
Mzize kwa sasa ni Lulu hivyo hauzwi kwa hasara.