Rasmi uongozi wa Yanga SC umetangaza kwamba kuelekea msimu ujao wa 2025-2026, wachezaji nyota wake watano hawatakuwa sehemu ya kikosi hicho ikiwa ni mwendelezo wa maboresho ya kikosi hicho huku zoezi la kusajili nyota wengine likiendelea.
Nyota hao watano walioondoka Yanga na hawatakuwepo kwenye mipango ya timu kwa msimu ujao ni Aziz Ki ambaye ameuzwa, Wengine ni Khalid Aucho, Clatous Chama, Kennedy Musonda na Jonas Mkude.