Sakala la Mchezaji KIBU Denis Kufanya Majaribio Kimya Kimya na Kuitosa Taifa Stars Lipo Hivi

Sakala la Mchezaji KIBU Denis Kufanya Majaribio Kimya Kimya na Kuitosa Taifa Stars Lipo Hivi


Wakati ikifahamika kwamba nyota wa Simba, Kibu Denis ameenda mapumzikoni nchini Marekani, lakini taarifa zinabainisha anajifua na kikosi cha Kristiansund BK kinachoshiriki Ligi Kuu ya Norway kuangalia namna ya kujiunga na timu hiyo.

Wakati Kibu akiwa kwenye majaribio hayo ambayo arena inafahamu kwamba ni ya wiki mbili, Kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman Morocco ameziba nafasi yake kikosini akiendelea na maandalizi ya michuano ya CHAN.

Ipo hivi; Kibu ni kawaida yake kila msimu kwenda Marekani kwaajili ya kukaa karibu na familia yake na sasa inaelezwa kuwa amepata timu ya majaribio ya wiki mbili kipindi hiki ambacho alitakiwa kuwa Misri na Taifa Stars inayojiandaa na michuano ya CHAN itakayoanza Agosti 2 hadi 30 mwaka huu ikifanyika Tanzania, Kenya na Uganda.

Kibu anafanya mazoezi na Kristiansund BK, timu ambayo awali mapema msimu uliopita 2023/24 alishawahi kwenda huko na kufanya majaribio lakini biashara ya kuuzwa ilishindikana.

Chanzo cha kuaminika kutoka kwa rafiki wa karibu wa mchezaji huyo, kimenieleza kuwa, Kibu anafanya majaribio ya kimyakimya ili mambo yakienda sawa aufahamishe uongozi wa Simba kama biashara inaweza kufanyika.

“Kibu bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba, hivyo ni mchezaji halali wa timu hiyo, nafikiri anachokifanya huko uongozi wa Simba unafahamu kwa sababu sio kwa kificho kama msimu mmoja nyuma,” alisema mtoa taarifa huyo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad