Taarifa za Simba kuhusishwa na kutaka Kumsajili Kiungo Mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua Niza Uongo na hazina Ukweli wowote Ule.
Mnyama Simba hana Mpango wa Kumsajili Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ivory Coast kama ilivyoelezwa na kusambazwa katika Mitandao mbalimbali ya Kijamii.
Pacome Yuko Nyumbani kwao Ivory Coast kwa ajili ya Mapumziko mafupi baada ya kukamilika kwa Msimu wa Ligi 2024/2025.
Kabla Hajaondoka Nchini, Pacome aliongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia Wananchi Mpaka 2027.