HANS RAFAEL anasema kuwa “Ukisikia taarifa za Panga kubwa kupita Simba unapata wasiwasi kama kweli wanajenga timu au wanabomoa, Binafsi sidhani kama ni wakati wa kufukuza Wachezaji 10 na kusajili wapya 12”
“Kwa maoni yangu Simba wanahitaji Wachezaji wapya watano ambao TOP (Upgrade ya waliokuwepo)”
“Kwanza Simba wanahitaji “Surgery” (upasuaji) kwenye safu yao ya ulinzi (Che Malone na Karabou) watakufanya ushinde mechi mbili tatu ila hawatokupa ubingwa….Simba wanatakiwa kupata mabeki Wawili wa kati imara”
“Pili Simba wanahitaji viungo wawili (1) holding midfielder mwenye uwezo wa ku-control mechi na kuamuwa timu icheze vipi (Aucho type) (2) advanced playmaker Simba wanatakiwa kupata namba 10 mwenye uwezo wa kuchezesha timu eneo la mbele na kuleta ubunifu”
“Tatu Simba wanahitaji namba #9 mwingine “Gunman“ mwenye uwezo wa kukupa goli 20+ kwa msimu”
“Simba wakifanikiwa kupata hao Wachezaji watano 🔝 watageuka kuwa tishio….ila wakienda kuzoa Wachezaji average 17 wapya basi kila mwaka story itakuwa ni ile ile “Tunajenga timu” Amesema Mchambuzi Hans Rafael