Kaizer Chiefs Hawapoi Kwa Feisal, Watuma Offer Nyingine Kubwa Kwa Feisal Salim




Kwa mara ya kwanza, Kaizer Chiefs walituma ofa iliyotajwa kuwa ni $386,000 (Dola 368,000) sawa R7 milioni kwa Azam ili kumnunua Feisal Salum, taarifa kutoka Afrika Kusini zimeripoti.

Azam, hawakuonesha nia ya kumuachia Feisal, lakini waliacha milango wazi endapo tu ile ofa waliyokua wakiihitaji itafikiwa na Feisal Salum anaweza kuondoka kwenda Kaizer.

Ofa ya sasa ya Kaizer Chiefs inatajwa kuwa ni R40 milioni. Wawakilishi wa Feisal Salum wanatajwa kusafiri kwenda Afrika Kusini jana kwa ajili ya mazungumzo hayo.

Inatajwa, kwenye mkataba wa Feisal na Azam kuna kipengele cha 25% ya fedha za mauzo ya Feisal, zitakwenda Yanga kama sehemu ya makubaliano ya mauziano kati ya Yanga na Azam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad